Monday, 4 June 2018

Shamsa awafungukia akina Wolper


MWANAMAMA wa Bongo Muvi, Shamsa Ford amewavaa na kuwaponda wakongwe wenzake wa tasnia hiyo kwa maelezo kwamba hawana jipya hivyo kutaka sura mpya kujitokeza kwenye fani hiyo.

Shamsa alifunguka ishu hiyo wiki iliyopita alipokuwa akifanya usahili wa wasanii chipukizi watakaouza nyago kwenye sinema mpya iitwayo Saa Imetimia inayoratibiwa na mdau wa Bongo Muvi na mwanaharakati, Lilian Wassira.

Shamsa aliwataja mastaa wakubwa kama Aunt Ezekiel, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na wengineo kuwa wanashindwa kuonesha jipya kwenye tasnia hiyo na kuwafanya mashabiki kuhamia kwenye sinema za nje.

No comments:

Post a Comment