Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu), George Mkuchika amewataka wasioridhishwa na utendaji kazi wa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kwenda mahakamani kutafsiri sheria.
 
Mkuchika ametoa kauli hiyo, leo Juni 8, 2018 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA), Ruth Mollel aliyeihoji serikali kuwa, Wakurugenzi wa Halmashauri ambao wameteuliwa wengi wao walikuwa ni wana CCM walioshindwa katika kura za maoni na wao ndio wasimamizi wa uchaguzi kuna wengine kama huyu wa Ubungo anahudhuria vikao vya CCM, Swali langu ikiwa tutaleta orodha ya Wakurugenzi ambao tunajua ni wana CCM na walikuwa katika kura za maoni Je serikali itakuwa tayari kuwaondoa?

“Swali la pili tunao wakuu wa mikoa ambao wanalipwa kwa pesa za walipa kodi Watanzania wenye vyama na wasiokuwa na vyama lakini wengi wameonyesha itikadi za kisiasa ukiangalia mkuu wa mkoa Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Manyara na wengine Je, serikali ina kauli gani kuhusu hilo?

Akijibu swali hilo, Mkuchika amesema kuwa “Mkurugenzi yoyote utakaye mchagua katika nchi hii lazima kuna Chama anachokipenda, huyu yuko pale baada ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi na Waraka wa utumishi wa umma unasema Mtumishi wa umma anaeteuliwa na Rais endapo hata ridhia kufanya ile kazi ana ruksa ya kumuambia Mh. Rais naomba niendelee na kazi yangu , sasa hao wakurugenzi walipokuwa wanafanya kazi walishakoma kazi waliokuwa wanaifanya, kazi wanayoifanya ni Ukurugenzi wa Halmashauri nataka niseme Rais anapoingia madarakani anapanga safu yake.”

Ameongeza, “Yule wa Ubungo kuhudhuria vikao naomba nisema mkishakuwa mnachama tawala siku zote kazi yenu nikuihoji serikali , Mkurugenzi wa Ubungo sio Mjumbe wa CCM lakini anweza kutwa akaelezea utendaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo la Ubungo.”

Amesisitiza kuwa “Swali la pili kuhusu wakuu wa mikoa , nataka niseme Wakuu wa Mikoa wanamuwakilisha Rais, Mkuu wa Mkoa ndio Rais wa Mkoa ule , Rais ni neno la kiarabu maana yake kichwa kwahiyo kichwa cha mkoa ule ni Mkuu wa mkoa ule, huyu Mkuu wa Mkoa anamuwakilisha Rais , hutegemei huyu Mkuu wa mkoa afanya mambo tofauti anayofanya Rais, lakini mwisho nimalizie kusema kwamba nchi hii tunachombo kinaitwa mahakama muhimili wa mahakama kazi yake ni kutafsiri sheria , pale mtu anavyoona hakutendewa ndivyo sivyo basi tufuate mkondo wa sheria na baadhi yao mnaowasema walikuja hapa kwenye maadili wakasiliza wakawa cleared wakaonekana hawana makosa.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: