Wednesday, 6 June 2018

Serikali Yalitaka Baraza la Maaskofu KKKT Kuufuta Waraka wa Pasaka

Serikali  ya Tanzania imelitaka Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Tanzania kufuta waraka lililoutoa wakati wa mfungo wa kwaresma kwa madai kuwa Baraza hilo halina mamlaka kisheria ya kutoa waraka huo.

Leo Juni 6, 2018 imesambazwa barua inayoonyesha imeandikwa na Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda kwa mwenyekiti /askofu mkuu wa KKKT iliyoandikwa Mei 30, 2018 ikitoa maelekezo ya kufutwa waraka huo ndani ya siku 10 tangu ilipoandikwa barua hiyo.

Ikiwa na kichwa cha habari ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa KKKT’ barua hiyo inaeleza baraza hilo halitambuliki kisheria katika ofisi ya msajili.


Aidha, barua hiyo inaeleza kuwa Katiba inayotumiwa na Kanisa hilo ni ya mwaka 1960 ambayo ilipitishwa na msajili mwaka 1963. Hivyo Serikali inalitaka Kanisa hilo kuomba kibali cha kufanya marekebisho ya katiba hiyo. 

==>Bado tunaendelea kufuatilia uhalisia wa barua hiyo ambayo iko hapo chini  na tutaendelea kukujuza.


No comments:

Post a Comment