Monday, 4 June 2018

Salum Mkemi ang’atuka, awataka viongozi waliobaki kujitathimini


Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga, Salum Mkemi ametangaza kung’atuka kwenye nafasi zake zote za uongozi ndani ya timu hiyo huku akiwataka waliyosalia kujitathmini kama wanafaa kuendelea kuvaa viatu hivyo.

Mkemi ametangaza kuachia ngazi hapo jana kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram mara tu baada ya klabu yake ya Yanga kupokea kipigo cha jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya timu ya  Kakamega Homeboyz.
Kusema Kweli Viongozi Hatukwepi Lawama Hizi
Kwa Hakika Tumepata Aibu
Kubwa
Nikiwa kama Kiongozi napaswa kuwajibika kwa Hili
Ni hatua nzuri ya kupisha Mawazo mapya kwa Wanachama wengine kuongoza Timu na Kutupeleka Mbele, pia ningependa kuwashauri Viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie Ngazi Ufanye Uchaguzi Mkuu kwa Pamoja tupate Viongozi wapya kabla msimu Mpya Haujaanza
Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikikwaza.
Naomba kutamka Rasmi Mimi Salum Mkemi
Nijaizulu nafasi zangu zote za Uongozi ndani ya Klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club “YANGA ” kuanzia tarehe ya Leo 03/06/2018
Nawatakia kila la kheri Viongozi wenzangu waliobaki na Kuwataka Radhi tena Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kwa Matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane.
Nawashukuru kwa Muda mlionipa kuiongoza Klabu hii kubwa Afrika
Naomba Kuwajibika kwa Kujiuzulu
Wenu Mwanachama Mwenzenu Mtiifu
SALUM MKEMI
NIMENG’ATUKA

Kwa matokeo hayo yameifanya Yanga kufungasha virago vyake na kurejea nyumbani Tanzania.

No comments:

Post a Comment