Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Amos Makalla ameunda tume ya watu nane na kuipa jukumu la kutembelea na kukagua miradi yote ya maji iliyopo kwenye halmashauri za mkoani humo.
 
Lengo la kuundwa kwa tume hiyo ni kubaini ubora na mapungufu kwenye utekelezaji wa miradi ya maji kutokana na kile kinachotajwa kuwepo kwa miradi iliyojengwa chini ya kiwango.
 
Miongoni mwa miradi inayotarajiwa kukaguliwa ni pamoja na uliojengwa katika kijiji cha Kiwanja kata ya Mbugani wilayani Chunya ambao unalalamikiwa na wananchi kujengwa chini ya kiwango kwa ufadhili wa Benki ya Dunia(WB).
 
Akizungumza katika maeneo na nyakato tofauti wilayani Chunya,Makalla amesema tume hiyo itapitia na kukagua mradi mmoja baada ya mwingine na hakuna utakaoachwa katika halmashauri zote.
 
Aidha amewasihi wananchi kwenye maeneo yote ya mradi kutoa ushirikiano kwa Tume hiyo ili iweze kukamilisha kazi yake kwa ufasaha na kwa wakati na kuiwezesha Serikali kuchukua hatua baada ya kazi kumalizika.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: