Saturday, 9 June 2018

Rc Makonda afturisha, aomba viongozi wa dini kufanya mambo haya


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini kuendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli kwani anafanya kazi ngumu na kitu pekee ni kuendelea kumuombea.

Amesema kwa nafasi ya Rais wapo ambao wanampenda na wapo ambao wanakasirishwa lakini cha msingi ni kuongeza maombi na Dia kwa Rais wetu huku akihimiza umoja na mshikamano. Makonda ametoa kauli hiyo leo jioni hii katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam kabla ya futari maalum ambayo ameiandaa kwa mamia ya wakazi wa Mkoa huo.


Amesema viongozi wa dini wana nguvu kubwa na ndio maana watu wanakwenda Kanisani, watu wanakwenda Msikiti na kueleza nguvu hiyo itumike kushirikiana na Serikali. Hivyo ameomba viongozi wa dini kuendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli ili aweze kulitumikia Taifa na kusisitiza nafasi anayoitumikia Rais ni kubwa na inahitaji maombi.

"Rais wetu anafanya kazi kubwa, na dua za viongozi wa dini ni muhimu ili aweze kulitumikia vema taifa letu. Kama mimi kwa nafasi yangu napigwa mawe hivi je kwenye nafasi ya Rais itakuaje? "Rais wetu anapongezwa na mataifa mengi kwa kazi nzuri anayoifanya na kwa hapa nchini wapo wanaopongeza kwa nguvu zao zote na wapo wanaomkasirikia.

"Sishangai wakitokea wa kubeza na ukwel ni kwamba wabadharifu wa fedha za umma hawawezi kufurahia, "amesema Makonda. Akizungumza siku ya leo kutokana na kuandaa futari hiyo Makonda amesema wapo viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa vyama vya siasa na makundi mbalimbali.


 Amesema anamshukuru Mungu kwa wananchi wote bila kujali dini zao wanaungana katika mwezi wa Ramadhan kuuheshimu.Amesema hakuna imani ya dini ambayo ameihasau kwani wote wamejumuika kwenye futar hiyo na kubwa zaidi ni kwamba hiyo inaonesha umoja na mshikamano Katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Amefafanua ktika futari hiyo kuna makundi mbalimbali wakiwamo wacheza mpira,wasanii wa Bongo Fleva, watu mashuhuri, na kila aina ya makundi ya wananchi. Makonda amesema kumewepo na tofauti katika baadhi ya watu ambapo amefafanua jambo kubwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam viongozi wa dini zote na waumini wote wamebaki kuwa wamoja.

Amesema wakazi wa Dar es Salaam hawana muda wa kulumbana katika mambo ya kidini kwasababu wameamua kuwa wamoja.Ameongeza katika kuhakikisha watoto waishio kwenye mazingira magumu nao kupata futari ameamua kuwapelekea huko huko wanakolelewa.

"Leo hii kwenye futar hii wote tumependeza kutokana na mavazi nadhifu na kwa umoja uliopo huwezi kujua kati ya Sheikh na ambaye si Sheikh. Hili ni jambo jema na kwangu linanifariji. Ameeleza Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa umefikia watu milioni sita na Wilaya ya Temeke ndio inaongoza kwa idadi ya watu.

Amefafanua idadi ya watu iliyopo inachangamoto zake kwani ongezeko la watu linachangia kuibuka kwa changamoto nyingine za kijamii.

No comments:

Post a Comment