Rais John Magufuli amesema haridhishwi na utendaji kazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) , kutokana na kushindwa kutoa mikopo kwa wakulima hali inayosababisha sekta ya kilimo kusuasua.

Rais Magufuli amesema hayo leo Juni 4, jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Programu ya kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP2), uliofanyika.

“Sijaridhishwa na utendaji kazi wa Benki ya Kilimo, utoaji wa mikopo kwa wakulima umekuwa wa kusuasua badala yake wamejikita katika kufanya biashara na benki nyingine.

“Nawasihi mbadilishe mwelekeo na kupunguza gharama za uendeshaji ili wakulima anufaike.

“Wakati mwingine Benki ya Kilimo ikitaka kukopesha inawatafuta matajiri wakubwa sasa nikisema siridhiki na utendaji wa benki hii mtanikatalia, kwani nimesikia pia mmekuwa mahodari katika kupeana mikopo wenyewe kwa wenyewe,” amesema Rais Magufuli

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewataka mabalozi walioko nje ya nchi kufahamu kuwa moja ya majukumu yao ni kutafuta masoko kwa ajili ya mazao yanayopatikana nchini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: