Monday, 4 June 2018

Pacha walioungana Maria na Consolata kuzikwa Jumatano


Pacha walioungana Maria na Consolata ambao walifariki dunia juzi usiku wanatarajiwa kuzikwa Jumatano katika makaburi ya viongozi wa dini ya Roman Katoliki, Tosamaganga Mkoani Iringa.

Akizungumzia ratiba ya maziko ya pacha hao, leo Juni 4, Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Richard Kasesela alisema wapo katika hatua za mwisho za maandalizi ya mazishi hayo, Pacha hao wanaandaliwa jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili huku misalaba ikiwa miwili na kaburi moja.

Amesema ibada ya kuaga mapacha hao itafanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha  Ruaha (Rucu) kuanzia saa mbili asubuhi kabla ya safari ya Tosamaga kwa ajili ya mazishi.

"Taratibu zinaendelea na tumekubaliana kutengeneza jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili, tutakuwa na misalaba miwil lakini watazikwa kaburi moja," amesema.

Kasesela amesema kuwa tayari ndugu wa pacha hao kwa pande zote mbili wamewasili na kwamba saa kumi jioni watakutana tena kupanga bajeti ya msiba.

No comments:

Post a Comment