Tuesday, 5 June 2018

Nsajigwa ang'atuka Yanga SC


Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga SC, Shadrack Nsajigwa ametangaza rasmi kuachana na wanajangwani hii leo baada ya kumaliza kandarasi yake aliyosaini kutumikia timu hiyo.

Hayo yamethibitishwa na Nsajigwa mwenyewe wakati alipokuwa anazungumza na eatv.tv mchana wa leo kupata uhakika wa juu ya taarifa ambazo zilizokuwa zimezagaa kila kona kuhusiana kuachana na wanajangwani hao.

"Hizo taarifa ni za kweli kabisa, na nimechukua maamuzi hayo baada ya mkataba uliisha muda mrefu tokea siku Ligi Kuu Tanzania Bara ilipomalizika kwa msimu wa mwaka 2017/18", amesema Nsajigwa.

Ndani ya juma hili, Shadrack Nsajigwa amekuwa kiongozi wa pili kuondoka Yanga SC ambapo wa kwanza alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji Salum Mkemi

No comments:

Post a Comment