Thursday, 7 June 2018

Nandy adai amekatazwa na Boyfriend wake kumzungumzia Bill Nass

Msanii wa muziki Bongo, Nandy amedai kuwa amekatazwa na Boyfriend wake kuzungumzia kile kilichotokea kati yake na Bill Nass.

Muimbaji huyo ameiambia U-Head, Clouds FM kuwa hata alipokuwa katika media tour nchini Kenya ni kitu ambacho alikuwa anaulizwa mara kwa mara na kukiri kuwa kilikuwa kinamsumbua.

“Kawaida nimefanya interview hayo maswali yalikuwepo, hakikuwa kitu kidogo kilienda mbali sana na kilinisumbua kiukweli lakini yameshapita,” amesema.

“Unavyoniuliza maswali sijui ya Bill Nass nimeshakatazwa na Boyfrind wangu kuyaongelea mambo hayo,” amesisitiza Nandy.

April 12, 2018 Nandy na Bill Nass walikamata headlines za kiburudani Bongo hasa katika upande wa udaku kufuatia kuvuja kwa video yao ikiwaonesha wakiwa faragha. Suala hilo lilifika hadi bungeni na polisi waliweza kuwahoji wahusika.

No comments:

Post a Comment