Thursday, 7 June 2018

Naibu Spika amzuia Waziri Mkuu kujibu swali la waraka wa KKKT


Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson amemzuia Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kujibu swali aliloulizwa na Mbunge Vunjo, James Mbatia kuhusu agizo la Serikali kwa Kanisa la Kilutheri kufuta waraka wake

Naibu Spika alitoa zuio hilo kwa Waziri Mkuu huku akitumia mfano kuwa Spika wa Bunge alishawahi kumzuia Mbunge Saed Kubenea kujibiwa maswali yake yanayohusu dini.

Mbunge wa Vunjo, James Mbatia alitaka kujua Serikali inatoa tamko gani juu ya nyaraka hizo ambazo zimezua taharuki kwa jamii hasa ukizingatia Makanisa ni wadau wakubwa wa amani na maendeleo katika jamii.

No comments:

Post a Comment