Wednesday, 6 June 2018

Mzazi mwenzie na Shilole, Elias Makala ambaye wamepata bahati ya kuzaa naye mtoto wake wa kwanza amefariki dunia ghafla huko Igunga mkoani Tabora.
Shilole na marehemu Elias
Shilole amethibitisha taarifa hizo kwa kusema kuwa mzazi mwenzie amefariki ghafla baada ya kutoka kwenye starehe usiku wa kuamkia leo ambapo amekiri kuwa alikuwa haugui.
Shilole amesema kuwa marehemu alikuwa mzima wa afya na mara ya mwisho kuwasiliana naye ilikuwa ni miezi miwili iliyopita.
Marehemu Elias na Shilole wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaje  Joyce Godfrey (14) ambaye pia ndio mtoto wa kwanza wa Shilole .

No comments:

Post a Comment