Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Arusha Ndg. Saitoti Zelothe leo amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Arumeru.

Katika ziara hiyo Ndg. Saitoti amekutana na Vijana wa Ccm, Viongozi wa Chama na Serikali na Ametembelea miradi mbalimbali ya Vijana na kupokea Taarifa kazi ya Uvccm Wilaya.


Pia Ndg. Saitoti amewasihi viongozi kutatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo yao na kuacha kukaa maofisi, huku akiwataka watumishi wa Serikali kuendelea kukitangaza Chama kwa kazi nzuri,na maendeleo ya kila siku yanayoendelea kuletwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Rais Magufuli.


Kwa upande wake Katibu Hamasa wa Mkoa Ndg. Omary Lumato amewataka vijana kuhakikisha Vijiji na Vitongoji vilivyopo upinzani  vinareshwa ndani ya chama cha mapinduzi Ccm ifikapo 2019,Pia aliwataka viongozi wa wilaya kushuhulikia swala la ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali ya Arumeru.


Huku akiwataka  Viongozi wa Uvccm Wilaya ya Arumeru kuhakikisha wanaanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuondoa utegemezi kutoka Mkoani na Taifa na kwa kuanzia Hamasa wa Mkoa ametoa Mifuko Ishirini (20) ya Cement.


Pia Mwenyekiti wa Uvccm alimuunga mkono Katibu Hamasa wa Mkoa kwa kuchangia mifuko Ishirini na mitano  (25) ya cement.


Kwa Upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arumeru Bi. Hamisa Chacha aliwaahidi Vijana hao kuchangia mifuko kumi (10) huku wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa  wamechangia mifuko Arobaini na Saba (47) pamoja na Mabati Ishirini (20)

Share To:

msumbanews

Post A Comment: