Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema ushiriki wa Simba katika Michuano ya Sportpesa ni alama kwa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro leo, Dk. Mwakyembe amesema hatua ya Simba kushiriki fainali ya michuano hiyo sasa inakwenda kuitangaza Tanzania kwenye medani za kimataifa.

“Ushiriki wa Simba kwenye michuano ya Sportpesa ni alama kwa nchi yetu, kwa sababu akishinda anakwenda kucheza na Everton ya Uingereza.

“Nami nilikuwa nafikiria kwenda kushuhudia fainali hizi nchini Kenya, lakini acha tuone kwanza. Hapa lazima tuweke uzalendo mbele kwa Simba ambayo inawakilisha Tanzania kwenye michuano hii, ” amesema Dk. Mwakyembe.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: