Tuesday, 5 June 2018

Mnyika Aihoji Serikali Kuhusu Wafungwa Wanaobambikiziwa Kesi

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema) ameitaka Serikali ieleze ni lini itaanza kutoa fidia kwa wafungwa waliobambikiziwa kesi.

Akiuliza swali la nyongeza Bungeni leo Juni 5, kwa niaba ya Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mnyika alidai kwamba katika gereza la Segerea wafungwa wengi wamekuwa wakibambikiziwa kesi.

“Je, Lini Serikali itaanza kutoa fidia kwa wale waliobambikiziwa kesi,” aliuliza Mnyika.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Wizara ya Sheria na Katiba, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde alisema utaratibu wa kimahakama upo wazi kwa wale wanaobambikiziwa kesi kufungua kesi ya madai.

No comments:

Post a Comment