Monday, 11 June 2018

Mkuu wa Mkoa Alazimika Kutumia Helkopita Kukagua Maeneo Yalizingirwa na Maji ya Bwawa la Nyumba Mungu

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira Jana Jumapili Juni 10, 2018 ametumia helikopta kuzunguka baadhi ya vijiji vya wilaya ya Same ambavyo wananchi wake zaidi ya 2500 hawana sehemu za kuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji.

Maji hayo yanadaiwa kutoka katika bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo siku za hivi karibuni limejaa maji kupita kiasi na kusababisha kuingia katika maeneo ya makazi.

Mei 19, 2018 vijiji vya Marwa na Ruvu Darajani vilifurika maji na kusababisha watu 2500 kukosa makazi baada ya nyumba zao kujaa maji, leo Juni 20, 2018 kijiji kingine cha Ruvu Jitengeni kimezingirwa na maji na kusababisha watu 300 kuzihama nyumba zao.

Walioathiriwa na maji hayo kwa sasa wamehifadhiwa katika kambi ya za Bagamoyo na Rolesho.

Mghwira tangu saa 6 mchana Jana alianza kuzunguka na helikopta kutembelea maeneo hayo ili pamoja na mambo mengine kubaini sababu za maji hayo kuongezeka wakati maji kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu yameanza kupungua.

No comments:

Post a Comment