Monday, 11 June 2018

MKUTANO WA WADAU WA KUJADILI MPANGO WA KUANZISHA PROGRAMU YA MASOMO YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA CHUO CHA NESLON MANDELA,


Kutokana na Sera ya Taifa ya teknolojia ya nyukilia (2013) inayoelekeza kuwepo na mkakati wa kukuza na kuendeleza uwezo wa rasilimaliwatu katika teknolojia ya nyuklia, Taasisi ya Nelson Mandela Arusha ikikishirikiana Tume ya Nguvu za AtomikiTanzania kupitia Shirika la Kimataifala Nguvu za Atomiki (IAEA) kwa pamoja wanaendesha Mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa kuanzisha programu ya masomo na utafiti za uzamili na uzamifu ya teknolojia ya nyuklia.

Mkutano huu umeanza leo tarehe 11/06/2018 katika Taasisi ya Nelson Mandela na utafikia kilele siku ya ijumaa tarehe 15/06/2018. 

Lengo kuu la mkutano ni kujadili jinsi utafiti na mitaala ya teknolojia ya nyuklia inavyoweza kuimarishwa ili kukidhi mahitaji ya kuendeleza teknolojia ya nyuklia nchini.

Namna gani utafiti na mitaala itajikita katika kuendeleza matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo katika Nyanja za Kilimo, uendeleaji wa Mifugo, Afya, Viwanda, Maji, Mazingira,uchimbaji wa Madini na Nishati.

Pia wadau watajadili changamoto zilizopo ili kuhakikisha kuwa matumizi ya teknolojia ya nyuklia yanachangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Imetolewa na;
Peter G. Ngamilo,
Kitengo cha Mawasiliano, Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: