Thursday, 7 June 2018

Mastaa Bongo baada ya kifo cha Sam wa Ukweli


Taarifa za kifo chake zimeshtua wengi kwani hakukua na taarifa za kuugua kwake hapo awali. Wasanii wenzake wameonesha kuguswa na kifo chake, hivi ni baadhi ya walivyoandika katika mitandao.
  • diamondplatnumzMBELE YAKO NYUMA YETU SAM…. InshaAllah Mwenyez Mungu ailaze Roho yako na za wote walotutangulia Mahala pema peponi Amin….๐Ÿ™๐Ÿป
  • niitesongaUlihakikisha kila aliyebahatika kuzungumza na wewe unamuachia furaha na kitu cha kujifunza,Daaah ngumu kuamini kuwa hatuko nawe tena ila hatuna budi..Mungu akulaze pema SAM WA UKWELI
  • kalajeremiahpUMZIKA KWA AMANI NDUGU YETU KIJANA MWENZETU MSANII MWENZETU SAM WA UKWELI UMEUMALIZA MWENDO. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Sam wa Ukweli amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Hospital ya Palestina, Sinza na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala Dar ss Salaam. Sam wa Ukweli alitamba na nyimbo kama Sina Raha, Kwetu Wapo na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment