Mkutano Mkuu wa klabu ya Yanga unafanyika kesho kwenye Ukumbi wa Police Officers Mess, Oyster Bay kuanzia saa 3 kamili asubuhi.

Kuelekea mkutano huo, taarifa zinasema aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Mfanyabiashara, Yusuph Manji, amekubali kuhudhuria mkutanoni ili kujumuika na wanachama wa klabu hiyo.

Mkutano huo unaenda kufanyika huku malengo makubwa yakiwa ni kubadilisha mfumo wa uendeshwaji wa klabu hiyo kutoka mfumo wa unaotegemea wanachama na badala yake kuwa wa uwekezaji.


Mbali na Manji kuhudhuria, Waziri aliye na dhamana ya michezo, Harrison Mwakyembe naye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kufuatia kualikwa na viongozi wa Yanga.

Uongozi wa Yanga umewaomba wanachama kufika mkutanoni wakiwa na kadi zao zikiwa hai ili kuweza kuingia ukumbini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: