Friday, 8 June 2018

Manara aipiga mkwara Gor Mahia


Kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la SportsPesa Super Cup kati ya wenyeji Gor Mahia dhidi ya Simba, mabingwa wa soka nchini Simba wamesema hawawaogopi wapinzani wao ila wanachotaka ni kuchukua ubingwa na kwenda England.

Akiongelea mchezo huo wa jumapili, msemaji wa Simba Haji Manara ameeleza nia ya klabu hiyo ni kutwaa ubingwa huo ambao msimu uliopita ulichukuliwa na Gor Mahia kwenye ardhi ya Tanzania.

''Tunawaheshimu Gor Mahia ila hatuwaogopi tuna imani kubwa mechi itachezeshwa kwa haki na tutashinda maana lengo letu ni kuchukua ubingwa kisha kwenda kucheza na Everton nchini England kwahiyo hatutaki kuipoteza hiyo nafasi'', amesema.

Simba ilitinga fainali ya michuano hiyo kwa kuifunga Kakamega homeboys ya Kenya kwa penati 5-4, kwenye mchezo wa nusu fainali. Gor Mahia wao walitinga fainali kwa kuifunga Singida United kwa mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment