Mahakama yawaachia huru Wakurugenzi Jamii Forums - MSUMBA NEWS BLOG

Friday, 1 June 2018

Mahakama yawaachia huru Wakurugenzi Jamii Forums


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na Mwanahisa wa mtandao huo, Micke William kwa sababu hawana kesi ya kujibu.

Viongozi hao, wameachiwa huru na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 6 wa upande wa mashtaka na kuona ushahidi u─║iotolewa una mashaka na kwamba hauna mashiko.

“Nawaachia huru washtakiwa kwa sababu ushahidi uliotolewa hauna mashiko,” amesema Mwambapa

Katika kesi hiyo namba 457 Melo na Mushi wanadaiwa kulizuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi wake, kinyume na kifungu namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao Namba 14 ya mwaka 2015.

Watuhumiwa wanadaiwa kushindwa kutoa taarifa kuhusu mmiliki wa akaunti moja iliyosajiliwa JamiiForums huku wakijua kwamba jeshi hilo linafanya uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyochapishwa kielektroniki kwenye tovuti hiyo.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done