Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema), amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi alieleze bunge juu ya mazungumzo kuhusu mchanga wa makinikia yalikofikia.

Amesema pamoja na kwamba Waziri wa Madini, Angellah Kairuki hakugusia suala hilo, katika kitabu cha bajeti ya wizara hiyo kuna haja Profesa Kabudi kulieleza bunge juu ya mchanga huo kwa sababu wananchi wanata kujua kinachoendelea.

Kubenea ametoa hoja hiyo bungeni leo alipokuwa akichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Sisi tulitegemea Bunge letu tupewe taarifa ya kina kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na Acacia. Tuelezwe Sh424 trilioni ambazo ni Dola bilioni 190 tungepata lakini Bajeti nzima imekuja haijazungumzia na ripoti ya waziri hakuna kokote,” amesema Kubenea

“Kwa kuwa mmoja wa wajumbe ni Profesa Kabudi atuambie makinikia imefikia wapi, mchanga uliozuiwa bandarini upo, utakuwapo hadi lini, mchanga unasafirisha? Kiwanda cha kuchenjua kitajengwa lini?” amehoji

Kubenea amesema fedha hizo Sh424 trilioni zinapaswa kila Mtanzania apate matibabu, kuishi maisha mazuri kwa fedha hizo zinapatijkana lini?

 “Suala hili ni muhimu kuelezwa makinikia yako wapi. Mazungumzo yamefikia wapi, fedha zinapatikana lini ili tuipate. Tutajua kila wilaya, kata kitapata kituo cha afya, bajeti ya miaka kumi.”

“Fedha hizi ni nyingi sana na kama tumeibiwa, Serikali ijiangalie vizuri na ili kufikia malengo tusipige danadana tuimalishe Stamico itakayosimamia madini yetu,”amesema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: