Friday, 8 June 2018

Kubenea amlalamikia Naibu Spika kukataa swali la Mbatia


Mbunge wa Ubungo Said Kubenea amelalamikia suala la Naibu spika Dkt. Tulia Akson kukataa swali la   mbunge wa Vunjo James Mbatia lisijibiwe na waziri mkuu akieleza kuwa Naibu spika amekiuka taratibu za Bunge kwa kupitisha maamuzi ambayo sio sahihi.

Akizungumza na East Africa BreakFast ya East Africa Radio Kubenea amesema Dkt. Akson ametaja sababu alizowahi kuzitoa Spika Ndugai jambo ambalo sio la kweli kwa sababu Spika huyo alisema yeye kwa kupenda kuuliza maswala ya dini kwa hivyo suala hilo halifanani na swali aliloulizwa waziri mkuu hapo jana.

“Huu ni mwendelezo wa mamlaka za bunge kuporwa kwa maksudi na uongozi wa bunge kwani kanuni zinasema mbunge yeyote anayo haki ya kuhoji kwa waziri yeyote kuhusu mambo ya umma”, amesema Kubenea

Jana katika kipindi cha maswali na majibu Naibu Spika Dk. Tulia akson alikataa swali la James Mbatia lililohoji sababu za serikali kuwatumia barua baraza la maaskofu Tanzania KKKT ikiwataka waufute waraka walioutoa katika kipindi cha kwaresma.

No comments:

Post a Comment