Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Josephat Kandege akikagua jengo akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji
la Arusha .
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Josephat Kandege akitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya wakati akikagua
ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Josephat Kandege akipatiwa maelezo wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya
Wilaya ya Jiji la Arusha
Moja ya jengo lililojengwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Jiji la
Arusha.
..........................................................................................
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Josephat Kandege amepongeza usimamizi mzuri uliofanyika katika ukarabati na ujenzi
wa vituo vya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Jijini Arusha.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara hivi karibuni ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa vituo vya afya vya Nduruma kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Jiji
la Arusha na Kituo cha afya cha Usa River Kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Meru, Jijini Arusha.

Mhe. Kandege amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya Jijini
Arusha, na kuwapongeza kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo ni
imara na yanaendana na dhamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

“Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya katika Jiji la Arusha ipo vizuri na kazi inayofanyika
inaridhisha ukilinganishwa na fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa vituo
vya afya nchini.

Mhe. Kandege ametoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha miradi
inakamilika kwa wakati ili huduma za afya ziweze kutolewa kwa wananchi.

Amezitaka Halmashauri kutengeneza mazingira mazuri ya vituo vya afya nchini ikiwa ni
pamoja na kuweka uzio, kupanda miti hasa ya matunda ili kutengeneza mandhari
inayovutia kwa wagonjwa pindi wanapohitaji kuaptiwa huduma ya afya.

Akiongelea kuhusu vyumba vya kujifungulia wanawake wajawazito Mhe Kandege
ameelekeza chumba cha kujifungulia kitenganishwe kila kitanda ili kuwa na usiri wa
mama mjamzito anapojifungua.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: