Tuesday, 5 June 2018

Fisi wavamia Kijiji na kula Ng'ombe wawili kwa dakika 45


Wakazi wa kitongoji cha Chang’ombe kijiji cha Iligamba, Mwanza wamejawa na taharuki baada ya fisi kuvamia katika makazi yao na kutafuna ngómbe wawili kijiji hapo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo saa nane usiku ambapo fisi hao walivamia nyumbani kwa Dominic Mgisa mkazi wa kitongoji cha Changómbe na kutafuna ngómbe hao, Kwa mujibu wa Mgisa, fisi hao waliwatafuna ng’ombe hao na kuwamaliza ndani ya dakika 45.

“Niligundua kuwa mifugo yangu inaliwa na fisi baada ya kutoka nje kujisaidia, niliposogea nikaona fisi, nikaogopa wasije kunidhuru nikarudi ndani,” amesema

Baada ya kuona hivyo Migisa alisema alipiga kelele kuomba msaada kwa majirani lakini hakuna aliyejitokeza kumsaidia kwa kuwa wengi waliwaogopa wanyama hao.

No comments:

Post a Comment