Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa yeye kigezo kikubwa anachotumia kumpata mwanamke mwema wa kuoa ni kuangalia sura na sio tabia kama wengi wanavyosema.

Diamond akitetea msimamo wake kwenye kipindi cha Kaa Hapa kinachorushwa TBC 1, amesema kuwa mwanamke huwezi kumbadilisha sura kwa namna yoyote ile lakini tabia ni rahisi kumbadilisha.

Akielezea kuhusu kigezo hicho, Diamond amesema kama angetoa asilimia kwa vigezo vya sura na tabia basi asilimia 70 angetoa kwa upande wa sura na asilimia 30 zilizobaki ndio angeangalia tabia.

“Kiukweli tabia tunapenda lakini wakati mwingine sura nazo zina uzito wake, Kiukweli tabia mnaweza kuelekezana ila sura kuelekezwa mtaelekezana vipi?. Tabia tunajifunza kama alijifunza kuchukia atajifunza kupenda, sura atajifunza vipi?, Kwa mwanamke mimi naangalia sura kwanza , tabia tutaelekezana.“amesema Diamond Platnumz.

Hata hivyo, kupitia kipindi hicho Diamond Platnumz amefunguka kuhusu zile picha za faragha zilizovuja akiwa na Hamissa Mobetto kwa kusema kuwa walikuwa location wakirekodi kipindi cha TV.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: