Saturday, 9 June 2018

CHADEMA hatujawahi kushindwa uchaguzi – M/Kiti Bavicha

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, BAVICHA, Patrick Ole Sosopi amesema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakijawahi shindwa uchaguzi lakini ushindi wao unapokonywa.
Sosopi ameyasema hayo alipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za Mwananchi Communications Limited, ambapo amesema kuwa ushahidi mzuri ni uchaguzi wa Kinondoni sanduku liliibiwa mbele ya Polisi.
“CHADEMA hatujawahi kushindwa uchaguzi lakini ushindi wetu tunapokwa, ushahidi ni Kinondoni sanduku la kura linaibiwa mbele ya polisi na linarudishwa hakuna anayekamatwa, imani ya wananchi kwa CHADEMA ni kubwa sana,” alisema Sosopi.

No comments:

Post a Comment