Bodi na Menejimenti ya Benki Kuu yaTanzania (BoT) Leo inakutana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhojiwa juu ya tuhuma zinazowakabili.

Benki hiyo inatuhumiwa kutumia bima binafsi badala ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Mwenyekiti wa PAC Naghenjwa Kaboyoka amesema watakutana na BoT leo, ameyasema hayo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

“Leo tumewaita na tutakutana nao. Baada ya kukutana nao taarifa tutaiwasilisha kwa Spika kama alivyotuagiza," amesema Kaboyoka ambaye pia ni mbunge wa Same Mashariki (Chadema)

Tuhuma kuhusu BoT ziliibuliwa na mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga Juni 4, 2018 bungeni  katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango mwaka 2018/19.

Amlinga amesema BoT inatumia Sh 12 bilioni kwa mwaka badala ya Sh 1 bilioni kugharamia matibabu ya watumishi wake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: