Thursday, 7 June 2018

Bavicha: Vifo vya pacha walioungana Maria na Consolata vimeacha funzo

Baraza la Vijana la Chadema, (Bavicha) limesema viongozi hawana budi kushiriki kutoa huduma za afya kwa wananchi badala ya kusubiri pindi wanapofariki.

Akitoa salamu za rambirambi kufuatia vifo vya pacha walioungana, Maria na Consolata leo Juni 6, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrick Ole Sosopi amesema vifo vyao, vimeacha funzo kubwa kwa jamii na Serikali.

Amesema Taifa linapaswa kukubali kuwa kuna tatizo kubwa la huduma za afya na uduni wa mazingira hospitalini.

 “Kila mmoja wetu kwa nafasi yake awaombee wapendwa wetu hawa waliokuwa na vipaji na malengo makubwa katika Taifa, Maria na Consolata Mwakikuti, mbele yetu nyuma yenu, Mungu awape pumziko la amani.

“Bavicha wanatoa pongezi na shukurani kwa Kanisa Katoliki walioweza kuwalea katika kipindi chote cha uhai wao,” amesema Sosopi.

No comments:

Post a Comment