Saturday, 9 June 2018

Baada ya Kocha wa Simba kususia timu mjini Nakuru, Kaduguga aibuka


Baada ya Mfaransa, Pierre Lechantre, kususia timu mjini Nakuru ambapo wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameweka kambi maalum kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup, aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Mwina Kaduguga ametaja mbadala wake.

Kaduguda anayejulikana kwa jina maarufu la Simba wa Yuda kutokana na mahaba yake makubwa ndani ya mabingwa hao wa mara 19 katika Ligi Kuu Bara, ameshauri aina gani ya kocha anayetakiwa kuinoa timu hiyo.

Kaduguda amefunguka na kueleza kuwa Simba ya sasa inahitaji aina ya Kocha atakayeisaidia Simba kuioa mwonekano mpya kulingana na falsafa yake.

Kwa mujibu wa Radio One, Katibu huyo wa zamani ameeleza kuwa Simba inahitaji Mwalimu ambaye ataweza kuifanya timu iwe bora haswa kwa wachezaji ambao wapo ndani ya kikosi.

Ameongeza kuwa aina ya kocha atakayekuwa na mabingwa hao wa msimu uliomalizika hivi karibuni, anapaswa kuifanya timu ioneshe utofauti pale inapocheza na timu za kawaida kama Stand United, Ndanda na zinginezo ili kuonesha kuwa hazina usawa.

Kaduguda amesema kuwa Simba ya sasa ikicheza na timu ndogo inashindwa kuonesha utofauti hivyo ni bora akaletwa Kocha ambaye ataweza kuipa sura mpya ya kuonesha ukubwa na thamani kama ambavyo jina lake lilivyo.

No comments:

Post a Comment