Sunday, 3 June 2018

ALIYEITESA YANGA ATUA SINGIDA UNITED NA KUSAINI MIAKA MITATU


Mshambuliaji aliyekuwa akiitumikia Mbao FC msimu uliomalizika hivi karibuni katika Ligi Kuu Bara, Habibu Kiyombo, amejiunga na Singida United kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Kiyombo ameonesha uwezo mzuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho pamoja na ligi huku akikibukwa kwa kuadhibu Yanga katika mchezo wa raundi ya kwanza jijini Mwanza, ametambulishwa leo baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezaji amekuwa mfungaji bora wa mashindano hayo baada ya kufikisha jumla ya mabao sita pekee.

Kiyombo ameungana na Singida United huku akipishana na Kocha Mholanzi, Hans Van der Pluijm ambaye ameaga rasmi klabuni hapo kuelekea Azam FC.

No comments:

Post a Comment