Friday, 8 June 2018

Alikiba ajibu tuhuma za kutowaposti Mastaa kwenye kurasa zake wanapofariki


KAULI ya Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba aliyofunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kutowaposti wasanii au watu maarufu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii wanapofariki akisema dini yake haimruhusu kumposti marehemu imepokelewa kwa mitazamo tofauti na mashabiki na wadau mbalimbali wa sanaa na mitandao ya kijamii nchini.

Kufuatia kauli hiyo inayotrendi mitandaoni, baadhi ya wadau wamehoji iwapo dini anayoisema inamruhusu kuzaa watoto wanne nje ya ndoa na kila mmoja akawa na mama yake, au ina mruhusu kufanya sanaa ya muziki, kutembea na wanawake na kuwaacha na mambo mengine mengi ambayo yameendelea kuibuliwa mitandaoni kufuatia kauli yake hiyo.

Akizungumzia jambo hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyik jana Juni 7, 2018 jijini Dar es salaam, Alikiba alisema kuwa sababu kubwa ya kutoposti picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo amedai kuwa kufanya hivyo ni kinyume na dini yake ya kiislamu.

Siyo mara ya kwanza kwa Alikiba kutoposti misiba ya wasanii wenzake, alifanya hivyo hivi karibuni kwenye msiba wa aliyekuwa Video Queen, Agness Masogange lakini alihudhuria kwenye shughuli ya kuagwa pale Leaders Club.

Sam wa Ukweli alifariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment