Wednesday, 30 May 2018

Yanga yatoa ufafanuzi ishu ya Tshishimbi kumalizana na Simba


Baada ya kuenea kwa tetesi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi kuhusishwa kuwa ameshamaliza na Simba, Yanga wameibuka na kutoa tamko.

Mkuu wa Idara ya Habari ndani ya Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa taarifa hizo hazina uhalisia wowote na anachokijua Tshishimbi alipowasilia Yanga alisani mkataba wa miaka miwili.

Ten ameeleza kuwa hana mengi zaidi ya kuzungumzia kuhusiana na Tshishimbi na badala yake amesisitiza akieleza kuwa Tshishimbi bado ni mchezaji wao.

Kiungo huyo mwenye asili ya Congo aliyewahi kuichezea Mbabane Swallows ya Swaziland alijiunga na Yanga Agosti 2017 na kusaini mkataba wa miaka miwili.

No comments:

Post a comment