Thursday, 3 May 2018

YANGA YAPANGIWA MUDA WA HATARI NA CAF KUKIPIGA NA RYON KOMBE LA SHIRIKISHO DARHuku mashabiki wakihofia miundombinu ya umeme na hali ya hewa ya Dar es Salaam, CAF imepanga mechi ya Yanga na Rayon ichezwe Mei 16, Saa 1 usiku.

Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumatano na CAF hupanga ratiba hiyo kutokana na haki za televisheni ambazo wanamiliki wao lakini hata klabu mwenyeji huruhusiwa kutoa maoni.

Kwa mujibu wa CAF mechi za Kombe la Shirikisho zitachezwa mara mbili kwa wiki ambapo moja itapigwa Jumatano na nyingine Jumapili. Jumamosi hakutachezwa mechi yoyote ya Shirikisho zaidi ya Ligi ya Mabingwa.

Hiyo itakuwa ni mechi ya kwanza ya Yanga kuchezwa usiku katika siku za hivi karibuni kwani nyingi zimekuwa zikichezwa mchana kutokana na miundombinu ya Dar es Salaam haswa kwenye suala la umeme.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten, amesema wameridhia muda huo ili kuruhusu mashabiki wengi waone mchezo huo na hawaihofii Rayon kwa vile wanaimudu.

Mechi ya Simba na Al Masry ya Kombe la Shirikisho ilipigwa usiku kwenye Uwanja wa Taifa umeme ukakatika na kuzua tafrani sambamba na mvua.

Kutoka Championi

No comments:

Post a Comment