Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako Leo ametembelea na kukagua hatua za mwisho za usimikaji wa vifaa mbalimbali ndani ya maabara ya kisasa ya Kuhakiki vifaa  vinavyopima  mionzi  katika Tume ya nguvu za Atomiki- TAEC iliyopo mkoani Arusha.

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara hiyo Waziri Ndalichako amesema serikali imejenga maabara  hiyo ya kisasa ili kudhibiti masuala ya mionzi kwa nchi za Afrika.

Alisema maabara hiyo ambayo sasa ipo katika hatua za kufungwa vifaa mbalimbali vya kisasa itawezesha nchi mbalimbali kuja kujifunza namna ya kupima masuala mbalimbali ya mionzi .

Waziri Ndalichako amesema  kuwa hadi sasa serikali imeshatoa kiasi cha sh. bilioni 2.38  huku  Umoja wa Ulaya (EU)  ikitoa vifaa vyenye thamani ya sh.  bilioni  11.

Imetolewa na;

kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

9/05/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: