Moja kati ya vitu ambavyo vinausumbua mchezo wa ngumi nchini Tanzania ni figisu figisu za mapromota wa ngumi pamoja na viongozi wa mchezo huo.
Hivi karibuni kuna tukio moja lisilo la kawaida limeripotiwa kutokea ambalo inadai kuna promota mmoja aliweza kumtoza pesa bondia kwaajili ya huduma ya choo ndani ya ndege.
Hayo amebainishwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa kwenye kikao maalum ya wadau wa ngumi nchini.
“Ngumi zetu zilipofikia ni aibu, hivi kweli promota unampeleka bondia kupigana nje halafu unamtoza chakula cha kwenye ndege? Na huduma ya choo? Huu ni uonevu mkubwa,”
Aliongeza, “Mabondia wengine wanapigwa ngumi za vichwani hadi wanapata matatizo, lakini bado mnawadhulumu, nimeshaambiwa hili na taarifa zake zote ninazo. Kuanzia sasa mikataba ya mabondia wanaokwenda kupigana nje sharti iwe wazi.”
Pia, hakuishia hapo amewaonya pia vigogo wa vyama vya ngumi nchini; Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustadhi’ na Rais wa PST, Emmanuel Mlundwa, kuwa wajitathimini kwa tuhuma zinazowakabili za kuvuruga ngumi za kulipwa nchini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: