Thursday, 10 May 2018

Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangala amewataka wabunge kutokubeza juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli ikiwemo ununuzi wa ndege kwani ni sehemu ya kipaumbele cha nchi

“Hakuna tatizo la kununua ndege kwani zinasaidia katika sekta ya utalii, kwani kuna watu wanasema mpango huo ni wa kukurupuka, sisi tulioko katika sekta hiyo tunakereka sana kusikia kauli hizo,” amesema Kigwangala.

Amesema Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi lakini inashangaza kuona inashindwa kuvitumia kutokana na kuwa na miundombinu mibovu ikiwemo katika shirika la ndege

Alisema nchi ya Ethiopia wamenunua ndege 10 kwa hiyo hakuna shida wala tatizo lolote kwa kununua ndege na akamuomba Rais kuendelea na mpango huo ili zinunuliwe ndege zaidi.

No comments:

Post a Comment