Wednesday, 23 May 2018

Wastara: Nawacheka wanaonitukana kuhusiana na afya yangu


STAA wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amesema kuwa, amejikuta akibaki akiwacheka wanaomtukana mitandaoni kuhusiana na afya yake kwani hawana jipya kwa sababu picha anazoposti ni za siku nyingi (TBT) alipokuwa India na hakuna wa kumzuia kuposti anachokitaka.

Akizungumza na Za Motomoto News, Wastara alisema kuwa, hakuna anayempangia cha kuposti na kinachomuumiza ni pale ambapo kuna watu wanachungulia akaunti yake kwa ajili ya kusubiri ataposti nini ili wamtukane.

“Sikuomba kuchangiwa ili nitukanwe, ilitokea tu kwa sababu ya matatizo. Kwa kifupi, wanaonitukana kwa sababu ya afya yangu, ninamuachia Mungu, kofi la Mungu ni kali sana maana sikuomba kuumwa ili nichangiwe na baadaye nitukanwe, ni mipango ya Mungu tu na atawaadhibu wanaofanya hivyo,” alisema Wastara.

Hivi karibuni, Wastara alitupia picha inayomuonesha amewekewa mirija kichwani akiwa nchini India ambapo picha hiyo ilishambuliwa kwa matusi huku wengine wakidai kuwa safari hii hawachangii bila kujua kuwa ni picha ya zamani.

No comments:

Post a Comment