Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka wale wote wanaoichafua serikali kwa kughushi vitabu na kuvitupia mtandaoni.
Prof. Ndalichako amesema kuwa katika mkutano unaoendelea jijini Dodoma unaojadili mapendekezo ya bajeti ya mapato na matumizi ya wizara mbalimbali kwa mwaka 2018/19 ambapo amesema huo ni uhalifu.
“Na mimi nimepata nafasi ya kuona kitabu cha Kiingereza cha darasa la tatu nikitabu kilichokuwa kina makosa ambayo yamekwisha kufanyiwa marekebisho na wahusika tayari wamekwisha kuchukuliwa hatua lakini pia kipo kitabu kinachosambaa ambacho kinaonyesha mwili wa binadamu na kwa kweli mishale ya yule binadamu imeenda ovyo ovyo , kitabu hicho hakijawahi kuwa sehemu ya vitabu vinavyotolewa na serikali na ninasikitishwa sana kwamba watu wameamua kutunga vitu vyenye lengo la kuichafua serikali na kufanya hilo ni kosa la jinai,” amesema Ndalichako.
“Nina furaha kwamba leo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipo hapa naviagiza mara moja vitafute watu ambao wanatengeneza vitu ambavyo vinaichafua serikali na kughushi na kuchafua serikali ili wachukuliwe hatua kwasababu wao ni wahalifu.”7
Share To:

msumbanews

Post A Comment: