Monday, 28 May 2018

WANANCHI WA SAMARIA WATAKIWA KUTOKUWA NA HOFU JUU YA ZOEZI LA UTAMBUZI WA MIPAKA YA UWANJA WA NDEGE KIAMwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru amewatoa hofu wananchi wa kijiji cha Samaria kuhusiana na zoezi la kutambua  eneo la uwanja wa ndege wa  kimataifa Kilimanjaro (KIA) kwa kuweka alama.

Mzava amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara ya wananchi hao uliolenga kufikisha ujumbe wa Serikali kuwa mnamo mwaka 1969 Serikali ilitenga eneo kwa ajili ya kiwanja cha ndege KIA na mwaka 1989 upimaji rasmi wa eneo hilo ulifanyika ambapo mwaka 2001 ilifanyika tathimini ya wananchi walioingia kwenye eneo hilo ambapo jumla ya kaya 289  zilionekana kuwa ndani ya eneo la uwanja huo wa KIA, hivyo Serikali imeamua kufanya tathimini ya kutambua  watu waliopo kwenye eneo la uwanja kwa kutambua eneo la uwanja na kuweka alama kwa lengo la kupata uhalisia na baada ya hapo itarudi kushauriana na wananchi kwa hatua nyingine.

Mzava ameenda mbali zaidi kwa kueleza kwenye Wilaya ya Arumeru jumla ya vijiji vinne baadhi ya maeneo yake yameingia kwenye uwanja ikiwemo kijiji cha Samaria ,Malula,Majengo kati  na Kaloleni hivyo amewaomba wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu na kutoa ushirikiano wakati wa utambuzi wa mipaka na kuweka alama kwani Serikali ni ya watu na ipo kwaajili ya watu  hawapaswi kuwa na hofu.

Wananchi wengi wameonesha kuwa na hofu na kutaka kufahamu hatma yao ikiwa maeneo yao yatakuwa kwenye eneo la uwanja wa ndege KIA na kujibiwa kuwa baada ya utambuzi wa kiwanja kufanyika na kujua nani yuko ndani ya eneo hilo na maendelezo yaalilomo Serikali itarudi kukaa nao jambo lililowatia moyo na kupungua kwa maswali.

Yonas Kimiree ambaye ni miongoni mwa wananchi ambao maeneo yao yanasadikika kuwa ndani ya eneo la uwanja wa ndege KIA amesema wananchi wanaimani na Serikali ya awamu ya tano kwa namna inavyofanya kazi hivyo hawana budi kukubali utambuzi wa eneo la uwanja kufanyika kwani wanatumai serikali itarudi kushauriana nao nini kifanyike
Nae Gadi Shami ameshukuru kwa ufafanuzi mzuri uliotolewa pia amesema wananchi hawawezi kupinga maendeleo na kuiomba serikali kuchukua maoni ya wananchi kuyafanyia kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher Kazeri ametoa rai kwa wananchi hao kutokushirikiana na watu wenye nia ovu ambao baada ya kusikia swala la utambuzi wa eneo la uwanja wanatafuta maeneo huko.
Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru akizungumza na wananchi wa kijiji cha Samaria
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher Kazeri akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Samaria
Afisa Ardhi Mteule kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Judas T. Mahuma akizungumza kwenye hadhara ya wananchi wa kijiji cha Samaria.
Wananchi wa Kijiji cha Samaria wakifuatilia kwa makini maelezo ya zoezi la utambuzi wa eneo la kiwanja cha ndege KIA
Wananchi wa Kijiji cha Samaria wakifuatilia kwa makini maelezo ya zoezi la utambuzi wa eneo la kiwanja cha ndege KIA
Wananchi wa Kijiji cha Samaria wakifuatilia kwa makini maelezo ya zoezi la utambuzi wa eneo la kiwanja cha ndege KIA
Mwananchi wa kijiji cha Samaria Gadi shami ameiomba Serikali kuzingatia maoni ya wananchi kwenye zoezi la utambuzi wa eneo la uwanja wa ndege KIA na hatua zitakazofuata.
Yonas Kimiree ambaye ni miongoni mwa wananchi ambao maeneo yao yanasadikika kuwa ndani ya eneo la uwanja wa ndege amesema wananchi hawawezi kupinga maendeleo hivyo wanaridhia zoezi la utambuzi wa eneo la uwanja wa ndege KIA kuendelea
Wananwake wakijiji cha Samaria wameiomba Serikali kuzingatia maoni ili hatma yao iwe ya heri.

No comments:

Post a comment