Like father, like son. Mtoto wa mchezaji Marcelo wa Real Madrid, Enzo Alves ameonyesha kufuata nyayo za baba yake tena kwa kiwango kikubwa zaidi.

Mtoto huyo ameonyesha dalili za kuja kuwa mchezaji wa soka ambaye anaweza kuwa hatari baada ya kuuchezea mpira na mastaa wa Madrid katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Enzo (9) alirushiwa mpira katika vyumba vya kubadilishi nguo katika uwanja wa Santiago Bernabeu na kuanza kuupiga kwa kichwa mara 13 bila kuuangusha kitendo ambacho kilimfanya kupata shangwe kubwa kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo akiwemo baba yake [Marcelo].
Share To:

msumbanews

Post A Comment: