WACHEZAJI zaidi ya 10 wa Yanga wamemaliza mikataba yao, na hofu imeibuka Jangwani kuwa huenda wengi wao wakatimkia Azam FC ambayo tayari imeshamkomba straika Donald Ngoma.

Azam imesema kuwa usajili wao wa safari hii utawashtua wengi, huku ikiaminika kuwa inataka kuwavuta kundini rundo la wachezaji wa Yanga.

Wachezaji ambao wame­shamaliza mikataba Yanga na wengine inamalizika hivi karibuni ni Kelvin Yondani, Hassan Kessy, Obrey Chirwa, Andrew Vincent ‘Dante’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Wengine ni kipa Beno Kakolanya, Emmanuel Mar­tin, Said Makapu, Geofrey Mwashiuya pamoja na Juma Abdul.

Mchezaji pekee ambaye anadaiwa kufanya mazun­gumzo ya kuongeza mkabata na uongozi wa klabu hiyo ni Yondani lakini bado hawajafi­kia makubaliano.

Hata hivyo, kuna taarifa kuwa uongozi wa Azam FC tayari umeshatia maguu na upo katika mazungumzo naye ya kutaka kumsajili yeye pamoja na wachezaji wen­gine wawili ambao ni Abdul pamoja na Chirwa.

Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu kuhusiana na wachezaji hao, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema: “Tuna­tambua kuwa kuna baadhi ya wachezaji wetu mikataba yao inafikia tamati hivi karibuni, hivyo taratibu kwa ajili ya kuwaongezea zimeishafan­yika.

“Tumeshazungumza nao na baadhi yao tumeshafikia makubaliano na wengine bado tunaendelea kuzun­gumza nao, kwa hiyo ni matumaini yangu kuwa mambo yatakuwa mazuri na niwaombe wapenzi na mashabiki wetu kutokuwa na wasiwasi.”

Akizungumzia kuhusiana na Azam FC kuwa katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji wao alisema: “Sina taarifa na hilo kwa hiyo siwezi kulizungumzia kwa sasa.”

Yanga imekuwa na tatizo kubwa la ukata lililofanya wachezaji wengi wagomee baadhi ya mechi za msimu huu kutokana na kuto­kulipwa mishahara, taarifa zinaeleza kuwa wengi wana­taka kuondoka kwa kuwa wanajua hakuna ‘mpunga’.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: