Wednesday, 23 May 2018

Wabunge washindi vijana wapokewa kwa shangwe Bungeni

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limewapokea wabunge washindi vijana, Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele na Mbunge wa Handeni Vijijini(CCM) Mboni Mhita.
Steven Masele alishinda kuwa Makamu wa kwanza wa Rais Bunge la Afrika na Mboni Mhita kuwa Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika.
Wabunge hao wametangazwa na kukaribishwa Bungeni leo, Mei 23, 2018 jijini Dodoma na Naibu Spika, Tulia Ackson ndani ya Bunge ambapo wapambe wa Bunge waliwapokea na kushangiliwa.
Mei 21 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliwapongeza Wabunge hao kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania huku akiwataka vijana kuiga mfano huo walipofika Ikulu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment