Saturday, 12 May 2018

Ushauri wa January Makamba wampa nguvu Flaviana Matata

Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Bongo, Flaviana Matata ameukumbuka ushauri aliowahi kupewa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba.

Flaviana amesema kuwa kuna kiongozi alimkwaza miaka michache iliyopita alitaka kulipuka akakumbuka ushauri wa waziri huyo aliowahi kumshauri kuwa asishiriki katika mizozo isiyo ya muhimu.

Kuna kiongozi alinikwaza sana miaka michache ilopita nkataka kulipuka nae Ila Kaka yangu @JMakamba akanambia “Choose your battles wisely Mdogo wangu” #ElimikaWikiendi,” ameandika Flavian Matata katika ukurasa wake wa kijamii.

Naye, Makanda alimjibu kwa kuandika “Si unaona heshima yako kwenye jamii bado ipo juu.”

Hata hivyo tofauti na Uana Mitindo Falviana Matata aliwahi kuwa Miss Universe 2007, hivi sasa Mjasiriamali wa bidhaa za kucha ziitwazo Lavy product

No comments:

Post a Comment