Leo May 3, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kesi ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee haipaswi kufika July 10,2018 kabla haijatolewa uamuzi.

Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali, Patrick Mwita kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini hawana shahidi.

Wakili Mwita amedai kuwa hawana taarifa za shahidi, wamemtafuta hawakumpata, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameueleza upande wa mashtaka kwamba kesi hiyo haipaswi kufika July 10, 2018 iwe imetolewa uamuzi.

Katika kesi hiyo, Mdee anadaiwa July 3,2017 katika makao makuu ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni alitoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwamba “Anaongea hovyo hovyo, anahitaji afungwe break”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: