Saturday, 5 May 2018

UONGOZI NDANDA WASEMA SIMBA WAKO VIZURI,Kikosi cha Ndada FC tayari kimesahawasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa ligi kesho dhidi ya Simba SC.

Simba itakuwa mwenyeji wa pambano hilo la ligi litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa majira ya saa 10.

Kuelekea mechi hiyo, uongozi wa Ndanda umesema wanaiheshimu wakieleza Simba na iko vizuri kwa sasa.

Ndanda wameeleza kuwa Simba wapo vizuri zaidi msimu huu ukilinganisha na utofauti wa alama walionao kwenye ligi.

Mbali na hilo Ndanda wamesema kila timu inahitaji kupigania alama 3, hivyo watapambana kwa kadri iwezekanavyo kutokana na nafasi mbaya waliyonayo ya kushuka daraja.

Wakati Simba ikihitaji alama 5 kutwaa ubingwa, Ndanda ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 23 pekee.

No comments:

Post a Comment