Tuesday, 1 May 2018

TUVUTE SUBIRA, TANZANIA YENYE NEEMA INAKUJA


Na Dr. Anthony M. Diallo

Kuanzia mwaka 1978, ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Kenya, vilikuwa ardhi na mbingu. 

Tanzania ilijikuta katika vita, na baada ya vita ikajikuta mufilisi.

Fikiria Taifa lilihitaji dola milioni 300 tu hivi za kufufua uchumi, lakini ilishindikana.

Wakubwa walibana kila mahali, wakati huo Kenya haina kabisa changamoto zetu, wao wanazungumzia ukuaji ni ngapi mwaka huu, na utakuwa ngapi mwakani, sisi tulikuwa katika recession tukipambana kupata stimulus package ya kuturudisha katika hali yetu.

Taila lilijikongoja katika hali ngumu ambayo halijawahi kupitia kuanzia 1980 hadi 1985, karibu kila.shirika la umma lilikuwa na uwezo wa kujiendesha wa chini ya 40%.

Vijana wa sasa na hii saratani ya kutopenda kusoma, hawawezi kujua hayo.

Mwalimu alipoondoka, akina Prof Mbilinyi, washauri wa Mwalimu wa Uchumi, walimshauri Mzee Mwinyi akubali masharti ya IMF, ambayo Mwalimu aliyakataa.

Ilikuwa kazi ngumu sana, Mwinyi Mzee wetu huyu katika simulizi zake, alisema hakuwa akilala na alifikia hatua akajua anaweza kupinduliwa.

Wakati analazimika kukubali masharti ya IMF, duniani kulikuwa na maandamano dhidi ya masharti hayo hasa katika nchi za Amerika ya Kusini na Magharibi mwa Afrika.

Mzee huyu alilazimika kupiga moyo konde, waziri wake wa fedha akiwa Mzee Msuya, Bajeti ya kwanza ya kuridhia masharti ikasomwa.

Ndio wakati Bongo hii kuingia choo cha umma na kulipa kuliwashangaza sana watu, sera ya cost sharing ilisababisha Mwinyi akawa unpopular sana, lakini hakuwa na namna.

Alipewa hizo pesa lakini hali ilikuwa mbaya na zisingeweza kufanya kitu.

Mkopo wakati fulani ulilazimika kulipa mishahara, karibu mashirika yote ya umma na viwanda vilikwenda Hazina kuomba mishahara.

Hata hivyo uchumi ulianza kufufuka kwa namna ingine ya kupitia sekta binafsi, na serikali ikaanza kupata vikodi ingawa havikuwahi kuiwezesha kujiendesha.

Hadi mzee Mkapa anaingia Ikulu, alikuta mashirika karibu yote, yanakwenda kuomba mishahara hazina.

Mkapa alikwenda kujaribu kuomba mkopo wa stimulus package awamu ingine, akanyimwa, akatakiwa aeleze alizochukia Mzee Mwinyi zimekwenda wapi.

Mkapa akarudi, wasiojua wanamlaumu bure, akabuni mbinu mbili au tatu.

Mbinu mbili za kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali, ili mapato kidogo ya kodi yagharamie shughuli muhimu za Serikali.

Hapo ndio ikaja mbinu ya kutangaza ubinafsishaji wa mashirika karibu yote ya umma mnakumbuka kamati ya PSRC.

Mbinu ya pili, ikawa kupunguza wafanyakazi wa Serikali, mnakumbuka "redundance" lilikuwa neno maarufu sana.

Mbinu ya tatu, ilikuwa kurahisisha kuvutia uwekezaji wa nje, kwa kupunguza masharti ya uwekezaji.

Haya mambo ya wawekezaji migodini, na wanunuzi wa mashirika na viwanda kwa bei chee, ndipo yalipoanzia, japo wakati mwingine yanatangazwa kwa sura ya upigaji, wakati kwa wakati ule hakukuwa na namna.

Mkapa ndio aliondoka akamwachia Mzee Kikwete Serikali yenye uwezo wa kulipa mshahara wafanyakazi wake.

Mwinyi na Mkapa, walirithi Serikali isiyo na uwezo wa kulipa mishahara, JK na JPM ndio waliopata bahati hiyo ya kurithi Serikali yenye makusanyo yanayoweza kulipa mishahara.

Wakati huo wa Mwalimu baada ya vita, wakati wa Mwinyi na sehemu fulani ya wakati wa Mkapa, Taifa lilikuwa likijitahidi kujinasua katika mkwamo wa kiuchumi, wakati Kenya wanajadili ukuwe kwa kasi gani.

Hata hivyo kazi ya Mkapa mwishoni, JK na sasa JPM wataalamu wanakwambia, Kenya imeshaona ni swala la muda mfupi kuachwa kwa kasi ya ajabu katika uchumi. Tanzania ishaonesha kila dalili kuwa ndio next economic giant wa Afrika Mashariki.

Hata Kenya kwa kuliona hilo, imewekeza sana Tanzania na inategemea sana soko ya Tanzania.

Kwa hiyo promised future Tanzania ni dhahiri, tusiruhusu vichangamoto vidogo kuharibu kazi kubwa iliyokwishafanyika na inayofanyika.

#HapaKaziTu 
#TukutaneKazini 
#KaziZaidi2020

No comments:

Post a comment