Wednesday, 30 May 2018

Tunda na Casto Dickson Wadaiwa Kumwagana

Video vixen maarufu Bongo, Tunda Sebastian amedaiwa kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake mtangazaji wa Clouds Tv Casto Dickson.

Tetesi hizi za wawili hawa kutemana zilianza kusikika mara baada ya Tunda kufuta picha zote za wawili wao enzi za mapenzi yao.

Kipindi cha XXL cha Clouds Fm wanaripoti kuwa wawili hao wameachana na Tunda ndio kampa kibuti Casto lakini unaambiwa Casto bado anabembeleza bembeleza.

Tunda alipotafutwa kuthibitisha taarifa hiyo alikataa kuongelea Mahusiano Yake na Casto Ikiwa na pamoja kukataa kukubali kama wameachana au bado wapo wote.

Lakini pia Shilawadu wanaripoti kuwa Tunda baada ya kumwagana  na Casto alirudisha majeshi kwa mpenzi wake wa zamani Young Dee ambapo wamedai kuwa Young Dee kamuweka Tunda kama profile picture yake ya WhatsApp.

Tunda alikana taarifa hizo za kurudiana na Young Dee na kusema kamwe hatakuja kurudiana na Ex wake kwani akimaliza Mahusiano na mtu anakuwa amemaliza.

No comments:

Post a comment