Wednesday, 2 May 2018

TUCTA kuijadili kauli ya Rais MagufuliKatibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA) Yahaya Msigwa, amezungumzia kauli ya Rais Magufuli juu ya kutoongeza mshahara kwa wafanyakazi, jambo ambalo limeonekana kuibua hisia hasi kwa watu wengi wakiwemo wanasiasa wenza na wafanyakazi wenyewe.

Akizungumza na www.eatv.tv. Bwana Msigwa amesema wao kama wawakilishi wa wafanyakazi, wanakusudia kufanya kikao maalum kujadili suala hilo, na kisha kulijadili na seriali kuangalia njia mbadala na muafaka.

“Mambo ya mishahara ni mambo ya utatu yaani wafanyakazi, waajiri na serikali, na mambo haya yanahitaji kujadili kwenye bodi, wafanyakazi wangependa kila mwaka kama inawezekana wawe wanapandishiwa mshahara, kwa hiyo hilo tutalijadili kama wafanyakazi halafu badaye tutajadiliana nao serikali”, amesema Yahaya Msigwa.

Hapo jana kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Me Mosi yaliyofanyika mkoani Iringa kitaifa, Rais Magufuli amesema hatoongeza mshahara wa wafanyakazi kwa sasa kutokan na serikali kijukita kwenye uboreshaji wa miundo mbinu.

No comments:

Post a Comment