Timu ya Wasichana ya Tanzania inayoundwa na Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa Kituo cha TSC Mwanza wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia la Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu baada ya kuifunga Uingereza magoli 2-1.

Mchezo huo uliyopigwa kwenye dimba la klabu ya Lokomotive mjini Moscow nchini Urusi Tanzania iliibuka na ushindi huo mnono kupitia kwa wachezaji wake, Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari.

Kwa upande mwingine timu ya Brazili imetinga hatua ya fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya  Ufilipino.

Tanzania ambayo ndiyo mabingwa watetezi baada ya kulitwaa kombe hilo mwaka 2014, itaikabili Brazil kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kupigwa kesho kutwa huku mpaka sasa ikiwa imeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: